
Lagos, Nigeria
MSANII mwenye urembo wa aina yake Yemi Alade amealikwa kuhudhuria kwenye sherehe kubwa za ugawaji tuzo za Grammy za nchini Marekani zinazotarajiwa kufanyika Februari 14, mwaka huu kwenye ukumbi wa Staples Center, Los Angeles, Marekani.
Mwimbaji huyo ambaye pia hutambulika kama Mama wa Afrika alitumia akaunti yake ya Twitter kuwatangazia mashabiki wake juu ya mualiko huo mkubwa.
Yemi Alade alionesha kufurahishwa na mualiko huo ambao unatarajiwa kukusanya wasanii mbalimbali wakubwa duniani katika siku hiyo.
Nchini Nigeria ni Wizkdi tu ndiyo anayrtarajiwa kushindania tuzo kutokana na kushirikiana na Drake wa Marekani katika baadhi ya nyimbo ambazo zipo kwenye albamu ya View.
0 Comments:
Post a Comment