MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abubakar Shaaban ‘Q-Chillah’ amefunguka na kutoa ya moyoni kwa kumwagia sifa mpenzi wake kuwa ni mvumilivu.
Katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii ‘Instagram’ ameandika, hivi karibuni tunatimiza miaka miwili katika uhusiano wetu umekuwa mvumilivu mwenye hekima ni wanawake wachache sana dunia hii wenye moyo wa chuma ulionao.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Sungura, amedai mwanamke huyo ni mwanamke wa pekee kutokana na uvumilivu wake tofauti na wanawake wote Duniani.
“Tumepita njia nyingi, tumevuka vikwazo vingi tumepitia kila aina ya changamoto tumepigana vita zote na kushinda sisi ni wababe wa vita nakupenda sana mpenzi wangu, hivi karibuni utatoka juani na utajikuta kivulini naamini maana Mungu wetu yu mwema nakizuri zaidi anatupenda sana,” aliandika.
0 Comments:
Post a Comment