Friday, January 13, 2017

Ben Pol; Ndoa inaua kipaji cha msanii

MWANAMUZIKI nyota wa muziki wa R&B, Benard Paul ‘Ben Pol’ amefunguka na kuweka wazi mipango yake ndoa na kusema kwa sasa yeye kuoa bado kwani anataka kujipanga zaidi lakini pia hata ikifika wakati wa kuoa itabidi aoe kimya kimya.
Akizungumza Dar es Salaam jana alisema hata ikifika wakati wa kuoa ataoa kimya kimya kwani anaogopa asijekupoteza mashabiki zake kwenye muziki ambao huwa wanajipa moyo kupata nafasi hiyo.
“Mimi kuoa bado kidogo nafikiri itafika muda muafaka nitafunga ndoa, bado najipanga ila mimi naamini ndoa huwa ina tabia ya kuharibu kipaji kidogo kwa asilimia kadhaa,” alisema.


0 Comments: