
MKALI wa nyimbo za Burger Selfie na Masogange, Belle 9 amesema ngoma yake mpya ya Give it tome me hajamuiga Diamond na Darasa kama wengi wanavyosema kutokana na kufanana kwake vionjo na wimbo wa Salome.
Stori ipo hivi, Baada ya Belle kutoa wimbo huo kuna vipande kwenye wimbo huo vinafanana ikiwemo mdundo jambo ambalo lilisababisha mashabiki kumponda lakini sasa Belle amesema hajamuiga yeyote bali yeye alishatunga na kuurekodi ila akawa amechelewa kuuachia.
“ Diamond ni mdogo wangu siwezi kumuiga kwa chochote na mimi nilishaurekodi kitambo na hata ukisikiliza mashairi yangu na Salome hayaendani, kwa wafuatiliaji wazuri wa muziki watakubaliana na mimi kuwa sijawahi kuiga msanii yoyote tangu natoka,” alisema Belle 9.
0 Comments:
Post a Comment