Tuesday, January 10, 2017

Amber Lulu aibua upya bifu lake na Gigy Money

KING’ASTI anayesumbua kwenye video za kibongo, Amber Lulu amerudi kivingine katika bifu lake na staa mwenzake wa video, Gigy Money na kusema hawezi kuwa na urafiki nae hata siku moja kwani siyo mtu wa aina yake.

Ubuyu upo hivi! Amber amesema licha ya kwamba wote wawili wanafanya kazi zinazofanana lakini kamwe Gigy hawezi kumfikia yeye kutokana na ubora wake na kwamba siku ikitokea wakawa marafiki basi Gigy atajivunia sana na kutangaza kila mahali.
mrembo huyo ambaye kwa sasa amegeukia pia uimbaji alisema “ Gigy hawezi kuwa na rafiki kama mimi kwenye maisha yake, mimi siyo wa mchezo mchezo siku tu akiongea na mimi atajivunia na kutangaza kila kona, kwa ufupi yeye siyo wa aina yangu” alijinasibu Amber Lulu.


0 Comments: