Katibu Mkuu wa Chama cha
Waansihi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) Hassan Bumbuli,
Akizungumza katika Jukwaa la Sanaa, kushoto ni Maofisa kushoto ni Maofisa
kutoka Mfuko wa Pensheni wa LAPF ambao walizungumzia umuhimu wa Wasanii
kujiunga na Mifuko ya hifadhi ya Jamii.
Wasanii nchini wametakiwa kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
katika mifumo ya hiari kwa lengo la kujiwekea akiba ya kuwasaidia katika
masuala mbalimbali kwenye maisha baada ya kufikia hali ya kushindwa kufanya
kazi.
Akiwasilisha mada ya umuhimu wa wasanii na wadau wa sanaa
kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Afisa Utekelezaji wa Mfuko wa Pensheni wa
LAPF, Emmanuel Maishaa amesema katika kipindi hiki ambacho Serikali
imetoa uhuru kwa mifuko kusajili wanachama walio nje mifumo rasmi ya ajira ni
vyema wasanii kutumia nafasi hiyo kujiunga na mifuko na kujiwekea akiba.
“Tunafahamu kwamba si rahisi pengine msanii kupata fedha
kila mwisho wa mwezi, lakini kwa mfumo wetu LAPF tunatoa nafasi ya kuchangia
kadri unavyopata. Nadhani na mifuko mingine inautaratibu wake lakini LAPF
tumeliangalia hilo na kutoa nafasi nzuri zaidi ili hata msanii mwenye kipato cha chini kabisa aweze
kumudu kuchangia,” alisema.
Amesema kwa kujiunga na mifuko ya jamii hasa LAPF wasanii
wanaweza kupata faida nyingi ikiwa ni pamoja na kunufaika na mafao mbalimbali
yanayotolewa na mifuko hiyo hivyo kujiwekea mazingira mazuri ya baadaye au ya
kuwawesha kufanya mambo yao kwa urahisi baadaye.
Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa LAPF Kanda ya Mashariki, Emmanuela Meishaa (kushoto) kakifafanua jambo katika Jukwaa la Sanaa wakati alipowasilisha mada ya Umuhimu wa wasanii na Wadau wa sanaa kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii. Kulia ni Sarah Mushi, afisa Maendesho wa LAPF.
“Msanii anaweza kujiunga na mfumo wa hiari ambapo baada ya
mwaka mmoja LAPF inatoa nyongeza ya asilimia tano kwenye michango yake, na
anaweza kujitoa wakati wowote baada ya kutimiza mwaka mmoja, katika mfumo huu
kiwango cha chini cha kuchangiakwa mwezi ni shilingi 20,000/- ambapo msanii anaweza
kulipa kiwango hicho kwa awamu na kwamba kuna nafasi ya kulipia kwa mkupuo kama
amechelewa au kupitisha mwezi mmoja,” alisema
0 Comments:
Post a Comment