MPIGA gitaa la solo mahiri nchini Tanzania, Adoph Mbinga amesema ameikimbikia bendi yake ya zamani ya African Stars"Twanga pepeta"kutokana na kujawa na ubabaishaji katika uendeshaji wa bendi hiyo.
Mwanamuziki huyo alisema ameikimbia bendi hiyo kutokana na kuwa na mapungufu mengi,ikiwa ni pamoja na kuwa na mikataba mibovu na kusema kuwa alipojiunga na bendi hiyo aliambiwa kwamba yupo katika muda wa majaribio ambao alidai muda huu aliopewa wa kujaribiwa haukuwa na mwisho.
"Ni ubabaishaji kufanya kazi na bendi ile,nilichukuliwa pale bila kuwa na mkataba rasmi na uongozi wa bendi hiyo,nilichopewa ni maelekezo ya kuwatendea kazi tu na ndio maana nimeamua kazi katika bendi hiyo na kama siyo wao wamemfukuza kazi kama wanavyodai,"alisema.
Akielezea mkasa ambao ulipelekea kuwa na uvutano kati yao na uongozi wa bendi hiyo,Mbinga alidai kwamba msuguano huo ulianza baada ya yeye kuomba ampatiwe mkopo wa shilingi laki nne ili aongezee kupata kodi ya nyumba na akatwe pesa hiyo siku za mbele na alidai mara baada ya kupeleka maombi yake hayo,uongozi wa bendi hiyo,ulishindwa kumsaidia kiasi hicho cha pesa,na badala yake uongozi ulianza kumpiga danadana katika kunisaidia.
"Kilichopo pale pale ni ubabaishaji,watu wanafanya kazi bila kuwa na mikataba yenye maslahi kwao na ukionekana kudai maslahi yako vilivyo,unaonekana mkorofi" alidai.
Meneja masoko wa bendi ya hiyo,Martin Sospeter alidai Mbinga ametimuliwa katika bendi hiyo kutokana na kuwa mtovu wa nidhamu,ikiwa ni pamoja na kutega kushiriki mazoezi na wanamuziki wenzake. Mbinga ni mmoja waasisi wa bendi hiyo ambapo ameshiriki kutunga tungo kadhaa zikiwemo Bwana Kijiko,Kisa cha Mpemba na kushiriki kupiga gitaa la solo katika vibao kadhaa vya bendi hiyo.
Na James Nindi
0 Comments:
Post a Comment