Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Gerald Simba a.k.a Ras Lion amesema kimya chao cha muda mrefu na swahiba wake Michael Muhina a.k.a John Woka si cha kitoto.
Akichonga na burudanikilasiku ndani ya jiji Dar es Salaam alisema wamekuwa kimya kwa muda mrefu wakifanya utafiti na kuona ni jinsi gani muziki huo unataka. Alisema wamekuwa katika utafiti kwa muda mrefu na baadaa ya utafiti wao huo wameona na kutambua matatizo mengi ya kijamii ambayo yanahitaji ufumbuzi wao kupitia muziki.
"Tulikuwa kimya sana tukifanya utafiti na utafiti huo ulitupelekea kusafiri sehemu tofauti kuongea na watu na sasa tumekuja na kazi ambazo zinatokana na utafiti wetu" alisema Ras Lion. Msanii huyo alisema kwa sasa wamekuja na vibao kadhaa vipya vikiwa vimebaba ujumbe mbalimbali kwa nia ya kuelimisha jamii na hasa katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu.
"Kuna kibao kinaitwa Babu na ndani ya babu tunaongelea wosia wa hayati Mwalimu Nyerere,hivyo wananchi watapata kusikia kazi hii ndani ya albamu yetu mpya, Sumu ya Panya ambayo kwa sasa ipo sokoni"alisema.
Ras Lion alisema ndani ya albamu hiyo ambayo wamefanya kwa kushirikiana na shwahiba wake John Woka imeshaingia sokoni ikiwa na idadi ya nyimbo kumi na tano ikiwa imerekodiwa katika studio za Grandmaster jijini Arusha pamoja na studio za Sound Crafters ya jijini Dar es Salaam.
"Kukaa kimya sio tumeacha muziki bali tulikuwa na kazi ya utafiti na sasa,washabiki wetu wataweza kutusikia"alisema msanii huyo ambaye aliwahi kutamba na vibao vyake kadhaa kikiwemo Umasikini Huu.
Wednesday, September 29, 2010
TULIKUWA TUNAFANYA UTAFITI-RAS LION
Wednesday, September 29, 2010
No comments
Source: James Nindi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Comments:
Post a Comment