Unapokuwa unazungumzia muziki wa Kenya hutashindwa kumtaja mkali Lenson Njuki Wang'a ng'a a.k.a Mr. Lenny aliyetamba kipindi na kibao chake cha nyuma na wimbo wake ‘Amenipa juju’ alichomshirikisha Nameless.
Mr Lenny anasema kuwa muziki kwake aliuanza alipomaliza shule na katika kipindi hicho hakuwa na wazo kama siku moja atakuwa mwanamuziki mzuri ila rafiki yake Nelson Kiama a.k.a Dr ndiye aliyemshawishi kuanza.
“Huyu bro alinishawishi kuimba kwani yeye alikuwa akiimba na kuniambia mimi naweza kuimba na hapo ndipo tuliamua kuanzisha kundi letu na mimi nilifurahi kwani katika kipindi hicho sikuwa na chochote cha kufanya nikakubali kuanzisha nae kundi,”anasema Mr Lenny.
Msanii huyo amesema kuwa katika kipindi hicho waliendelea kuimba kwa kushirikiana ila baadae waliamua kila mtu kuimba mwenyeewe na yeye hapo ndipo alipoanza kuimba mwenyewe na hapo ndipo alianza kuwika akiwa peke yake na kuamini kuwa anaweza kuimba peke yake.
Kipindi wanaachana na mwenzake Nelson Kiama walikuwa wakipenda kuimba nyimbo zao kwa lugha ya kiingereza lakini yeye sasa kuchanganya kiingereza na Kiswahili kwani wazo la kufanya hivyo alilipata kwa baadhi ya wasanii wenzake wa Kenya na hapo ndipo alipoanza kufanyia kazi wazo hilo.
Mr lenny anasema huwa anapenda kuimba nyimbo za R&B kwa sababu anazipenda na huwa zinasikilizwa na baadhi ya wasanii wengi tofauti ila huwa anabadilisha ‘style’ ya muziki iliyopo kwa wakati huo inayofanya vizuri ili kuendana na wakati.
Kwa upande wa maisha yake hasa mambo ya ndoa alisema kuwa kwa sasa bado ila anae mpenzi wake wa siku nyingi na ana mpango katika maisha yake na anatarajia kumuoa hapo baadae mungu akipenda, kwani suala hilo halina haraka sana kutokana na mpenzi wake kumuamini.
Kukaa kimya kwa Mr Lenny sio kwamba ameacha muziki ila yuko katika maandalizi makali ya kuja na albamu yake ya pili mwakani kwani anataka kutoa albamu ambayo itawashika mashabiki wake vilivyo na studio anayofanya nayo kazi sio moja bali ni nyingi ili kuleta radha tofauti.
“Katika albamu yangu hii nitafanya na R.K. ''Robert Kamanzi'',kutoka studio ya Shammah boy,na pia Freddie wa Homeboyz na wengine wengi kwa sababu kufanya nao kazi watu mbalimbali tunaifanya kazi yangu kuwa kali na nzuri na itapendwa Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla,”alisema Lenny.
Mr Lenny anasema kuwa anapenda kuimba nyimbo za mapenzi kwani sio kitu kigeni kwa watu kwani mapenzi yalikuwepo hata katika biblia yapo hivyo mapenzi ni swala nyeti hata nabii Solomon aliandika nyimbo nyingi kuhusu mapenzi linalohusu mabaya na mazuri katika maisha ya binadamu ya kila siku hivyo wasanii wanapoandika nyimbo za mapenzi ni kawaida.
CL ilimuuliza kama siku moja angekuwa katika radio station angewasaidia vipi wasanii katika suala la muziki?”Kama ningekuwa katika radio ningefanya mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na kuwapatia nafasi wanamuziki wengi wanaopenda kusikiliza muziki kwenye radio,pili ningewapatia mawaidha kuhusiana na muziki wanaoufanya ili kukubalika katika jamii zote nchini, tatu ningekuwa na kipindi kinachocheza muziki kutoka Afrika peke yake ili kubuni na kuendeleza Afrika, nne ningejaribu iwezekanavyo kuanzisha Awards Ceremony kama vile ‘KORA AWARDS’ ama ‘MTV’ambayo inatambua wasanii na kuwapa motisha ili kueneza muziki duniani ili kuweza kufikia levo ya kimataifa,”alisema Mr Lenny.
Lenny aliwasisitiza mashabiki wake wakae wa Kenya, Uganda na Tanzania wakae mkao wa kula kwa kuisubiri albamu yake ya pili anayoiandaa ambayo itakayokuwa na vibao vikali wasiwe na shaka kwani mambo mazuri yanakuja.
Pia Mr Lenny ilimuuliza kama angekuwa Waziri wa Kenya angewasaidia vipi wasanii wa hapo nyumbani?” Kama ningekuwa waziri ningejaribu sana niweke mambo sawa ambapo kungekuwepo kwa adhabu kali kwa wale wote wanaofanya ‘pirating’ na kutoa mswaada mzuri na sheria ya Kenya ingetoa amri kwa radio zote za Kenya kucheza asilimia sabini ya nyimbo za Kenya,”alisema Mr Lenny.
Kwa upande wa mambo ambayo Mr Lenny hatayasahau katika maisha yake na yaliyomuumiza ni kuhusiana na uchaguzi mkuu uliofanyika Kenya ambapo kulikuwa na machafuko na ghasia mbalimbali na kusababisha maelfu ya watu wasiokuwa na hatia kudhurika bila makosa yoyote huku ndugu kwa ngugu wakichinjana bila kuwa na huruma kwa sababu ya kikabila ila kwa sasa mambo kama hayo alisema hayatatokea tena.
Alimalizia kwa kusema kuwa ana ziara nchini Kenya na nchi za jirani na baadae ataenda kufanya ziara Ulaya na kuaahidi mashabiki wake wakae mkao wa kula ili kusubiri ujio mpya wa albamu yake mpya kama alivyosema hapo awali.
0 Comments:
Post a Comment