Tuesday, June 1, 2010

KINACHONIKERA NI KUPENDA KUWAPA NAFASI WASANII WA NJE NA KUWASAHAU WA NYUMBANI- AVRIL

Dah! mkubwa natumai utakuwa unamapata mwanadada aliyemghalisha Ay katika Remix ya Leo, utakuwa unamjua namzungumzia nani, si mwingine bali ni Judith Nyambura Mwangi "Avril".alitupasha mawili matatu juu ya kazi aliyofanya na wasanii kwa Afrika Mashariki.

Dada Avril unaweza kutuchana umeshafanya kazi na wasanii wangapi ili watu mbalimbali wajue kimtindo. " Mimi ni msanii mpya kwenye industry ya Kenya na Afrika Mashariki so, nina wimbo wangu mmoja wa 'Mama', na nimeshirikiana na baadhi ya wasanii kama Jaguar (Kenya), Kenzo (Kenya), Trapee (Kenya), Moustapha toka kundi cha Deux Vultures (Kenya), Collo toka kundi cha Kleptomaniacs (Kenya), King Georges (Kenya), A.Y (Tanzania), LAM (Sudan).

Mkubwa unamjua nani alimshawishi kufanya kazi, si mwingine bali ni produza wake Lucas Bikedo ambaye anafanya kazi za kutosha kenya mpaka kuingia katika industry ya muziki kabisa kwa sababu alikuwa anafanya kazi kibao za 'background vocals'.

Unajua kwanini mkubwa wangu! si nilitaka kujua ilikuwaje mpaka akafanya kazi na Ay kwenye Remix ya Leo. " Nilijisikia nimebarikiwa sana kufanya kazi na A.Y kwani ni msanii mkubwa sana Afrika Mashariki na alinipa moyo kuhusiana na soko la muziki kwa East Afrika kama rafiki na ndugu kwahivyo akanifunza mengi sana.

Unajua watu wangu wa kitaa Avril anaweuka na kufanya ngoma zipi? nikutajie au nimuache ataje mwenyewe, si ndio itakuwa mzuka au." Ninapenda kufanya muziki aina ya Contemporary Urban kwani ainibani kufanya lolote nitakacho hisi kinanipendeza kwa kuandika muziki".

Inaweza kuwa mzuka au sio mzuka kiivyo,unajua kwanini si nilimuuliza kitu kinachomkera katika muziki ni hiki hapa. " Kinachonikera sana ni kupenda kuwapa nafasi wasanii toka ng'ambo na kusahau wasanii wetu wa hapa Afrika.
Pia sio vibaya kuwa na 'music radio stations' na runinga zikionyesha muziki wa Afrika pekee na kuacha kupiga muziki toka ulaya, lakini sio vibaya local content ikiwa chini ya asilimia hamsini.

Wakubwa unajua nini! unapokuwa mwanamuziki lazima utakuwa unamalengo yako ndio maana ukafanya muziki au mnasemaje waungwana, basi mwanadada huyu lengo lake katika muziki ni kufanya mwanamuziki atakaetambulika Afrika na dunia kwa ujumla ili aweze kuwa 'role model' kwa wasichana kama yeye tofauti na wanamuziki wengine.

Dah! kweli mwanadada huyo anavipaji kibao moja katika vipaji vyake nje ya muziki anaufanya ni mwanachuo wa Design katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Na pia atatumia ustadi wake wa design kwa kuboresha muziki wake na kuwa na brand yake kama Avril.

0 Comments: