Hii ni kwa wasanii wote wanao fanya music wa aina mbali mbali wenye kueleweka na kuleta maana, kueleweka na wenye maadili kwa watanzania wote.
Nimeona nitoe offer hii ili mradi wasanii wapate nafasi ya kutosha katika kuelimisha jamii kuhusu uchaguzi wa amani, faida ya kupiga kura na kuelimisha jamii kuhusu viongozi wanao tufaa katika jamii.
Naomba wasanii wajitokeze ili elimu na ujumbe ufike kwa jamii. Wasanii wa mikoani wanaweza kupiga simu au kuandika barua pepe kwanza ili kuwapa booking kabla kwa kuwaondolea usumbufu wa kusubiria ratiba.
Hii isiwe kwa wasanii kupata nafasi ya kumuimba kiongozi flani au mtu flani hatufai hapana sina dhumuni la kutengeneza nyimbo kwa ajili ya chama flani au kiongozi flani kwa jina lake.
Vile vile ipo nafasi ya vyama vinavyo pigania haki, katiba na uratibu wa uchaguzi kuwapa nafasi pekee ya kurecord chochote kuhusu uchaguzi kama matangazo, michezo au hata nyimbo tenzi na ngonjera zinazo husu uchaguzi.
Offer hii ni kuanzia tarehe 01June2010 hadi 01August2010, ila wasanii wajiandae vya kutosha kwani sina lengo la kumfundisha mtu au mtu kutaka kujaribu kuimba tu kwa sababu amesikia ipo nafasi ya kurecod bure hapana, naomba nafasi hii iwe kwa wasanii wanaojua kuimba na wenye mazoezi ya kutosha na wawe na nyimbo zilizoandaliwa kwa ufundi zaidi ambazo zitapata nafasi katika media zote.
Backyard Records inawajali watanzania na ndio maana tumeamua kutoa nafasi hii wakati muwafaka ambao watanzania wanahitaji elimu na hamasa kuhusu uchaguzi. Tupo Magomeni Moroko hoteli Mchinga A. Street barabara ya Kawawa na Uzuri Road. Email backyardrecords@hotmail.com simu +255713888779
Wako
Samuel Andrew Mbwana (Braton)
Producer Backyard Records.
0 Comments:
Post a Comment