Ebwana hii itakuwa imekaa vizuri sasa kwa kijana wa mkoa wa Mwanza ambaye ni msanii aitwaye SAJNA, kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la IVETA, na hii ni singo yake ya 2 baada ya kutoa singo ya kwanza mwezi Jan mwaka huu iliyokuwa inaitwa NADHIFA na
Video ya wimbo huu tayari imekwishatoka, imefanywa na kampuni ya KALLAGE PICTURES, locations ni Dar es salaam na Pwani. Kwa sasa yuko katika hatua za mwisho kuikamilisha album yake ya kwanza chini ya TETEMESHA RECORDZ.
IVETA ni wimbo unaotokana na hadithi ya kweli, iliyomtokea jamaa mmoja mwenyeji wa mkoa wa kagera, aliyekuwa na mpenzi anaeitwa Iveta anaeishi Bukoba mpaka sasa, kisha huyo jamaa akaja Mwanza kutafuta maisha, akawa anafanya biashara ya kuuza miwa, akaja kufahamu kuwa Sajna ni msanii, ndipo aliamua kumfata Sajna na kumweleza kisa chake na kumuomba amuandikie wimbo ili kumpa ujumbe mpenzi wake aliyemuacha Bukoba, Sajna akaamua kuandika wimbo huu.SONG'S DETAILS
Singer: SAJNA
lyrics composed by: SAJNA
arranged by: KID BWOY & SAJNA
Produced by: KID BWOY
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ
Sandu George (Kid bwoy),
Tetemesha Recordz,
+255 713 131073
sandumpanda@gmail.com
Mwanza
Track Name: IVETA
Singer: SAJNA
lyrics composed by: SAJNA
arranged by: KID BWOY & SAJNA
Produced by: KID BWOY
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ
Intro
Oh ooh, ey ye ye yo yoooohh
Oh oohh, we Iveta
ningojee dia, ningojee dia
tetemesha, bwoy
Verse 1
Najua moyo wako unahitaji raha, ila huku mjini karaha
baridii inaumizaa, wewe sweta ulileta mzaha
sijui jibu langu umepata, kuhusu Saj kuja kwenu kukubaliwa
isije kuwa hadithi na ndoto, walishanieleza mapenzi maji ya moto
najua kwamba unanipenda mimi
ubavu wa kushoto ningoje Iveta.
Chorus
Iveta kijijini ningojee mamaa, ningojee dia
huku mjini nakutafutia mama, nakutafutia dia
Iveta kijijini ningojee mamaa, ningojee dia
huku mjini nakutafutia mama, nakutafutia dia
Verse 2
Subira yavuta heri, nisubiri kwa kila lakheri mpenzi
kijijini nimemiss vitu vingi, mboga za majani machungwa matunda
pale nyumbani hadithi za babu, ndugu zangu na utani wa bibi
Iveta nisubiri mimi, tuunganishe familia yangu na yako
Iveta maa, i love u
Iveta maa, i need you
Iveta maa , i love you.
Chorus
Iveta kijijini ningojee mamaa, ningojee dia
huku mjini nakutafutia mama, nakutafutia dia
Iveta kijijini ningojee mamaa, ningojee dia
huku mjini nakutafutia mama, nakutafutia dia
Bridge
Eeh eh ehh eh, ningojee dia
Aah ah ahh ah, nakutafutia dia
Verse 3
Mjini sichoki kutafuta, angalau senti kuja kuzileta
Iveta nisubiri basi mimi, si unajua nakupenda sana wewe
wangapi huku mjini wanitaka, ila najua wewe ndio unaningoja
usiwe na shaka ningoje mama, Iveta wewe
usiwe na shaka ningoje mama, Iveta wewe
usiwe na shaka ningoje mama, Iveta wewe
Chorus
Iveta kijijini ningojee mamaa, ningojee dia
huku mjini nakutafutia mama, nakutafutia dia
Iveta kijijini ningojee mamaa, ningojee dia
huku mjini nakutafutia mama, nakutafutia dia
Outro
eh eh eh eeeeh, haa
oh ooh, ningojee dia wange
ningojee diaaaaaaaaaah, haaa
tetemesha, bwoy
END
0 Comments:
Post a Comment