Monday, February 1, 2010

Tetemesha yauanza mwaka 2010 kwa kishindo

Msanii BONTA
Studio ya tetemesha kwa mwaka huu wa 2010 imeachia ngoma mbili kali za wasanii TID ana Synttax chini ya produza Sandu George Mpanda a.k.a Kid Bwoy ya jijini mwanza.

Nyimbo hizo za wasanii hao ni pamoja na Huyu aliyoimba msanii TID akishirikiana na Chid Benz, Usiulizie chai ya msanii Syntax akimshirikisha Rama D huku kazi zote hizo zikifanywa na produza Kid Bwoy na kuongeza kuwa mashabiki wakae kupokea vitu vya nguvu kutoka studio ya tetemesha ya jijini Mwanza.

Ameongeza kuwa kuna msanii mwigine wa hip hop kutoka kundi la RIVER CAMP linaloongozwa na JOH MAKINI, anayejulikana kwa jina la BONTA a.k.a MGANGA WA MTONI kutoka A-Town, Arusha naye ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la NIONESHE alioshirikiana na HUSSEIN MACHOZI ambao ni maalumu siku ya wapendanao.

Cha kufurahisha na kitu kizuri zaidi ni kwamba BONTA ni Daktari wa Hospitali ya Isaka Kahama, lakini kwa sasa anasoma BACHELOR OF PUBLIC ADMINISTRATION IN HEALTH, MZUMBE UNIVERSITY MOROGORO na sasa anajiandaa kufanya video ya wimbo huu.

Bonta ameshatoa ngoma kadhaa zilizomuweka katika nafasi nzuri katika muziki wa hiphop hapa Tz, baadhi ni, MACHO YANGU na MTI WENYE MATUNDA.

0 Comments: