HII NI COVER YA ALBAM YAKE
Ebwana mkubwa hii inaweza ikawa imesimama zaidi toka pande za pale Mwanza kwa produza kid Bwoy baada ya kuachia wimbo mpya wa msanii Hussein Machozi unaokwenda ZA MWIZI 40, ambao ameuachia rasmi katika vituo vya radio.
Na wimbo huu unapatikana katika albamu yake ya KWA AJILI YAKO na wimbo huo ni wa tatu kwa kutoka katika album hiyo, nyimbo mbili zilizotangulia ni pamoja na KWA AJILI YAKO na UTAIPENDA.
Kwa sasa Hussein Machozi yuko katika hatua za mwisho za kutengeneza video ya wimbo huu katika jiji la Dar es Salaam kutoka kwa Adam Juma wa Visual Lab katika wiki ya kwanza ya mwezi Machi mwaka huu.
SONG'S DETAILS
Track Name: ZA MWIZI 40
Singer: HUSSEIN MACHOZI
Produced by: AMBA & KID BWOY
Written by: HUSSEIN MACHOZI
song arranged by: HUSSEIN MACHOZI & KID BWOY
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ / AB RECORDS
MASHAIRI YA ZA MWIZI
VERSE-1
Nilipokufata mara ya kwanza nilikwambia "I got no money",
jibu lako toka moyoni mwako ukasema "its okey",
Nilipokufata mara ya kwanza nilikwambia "I got no money",
jibu lako toka moyoni mwako ukasema "its okey",
Nilidhani nimepata kumbe nimepotea njia,
nikienda kazini night kumbe ndo yako tabiaaa,
kosaaaa, la kwangu mwenyeweeee,
kumweka chui kwenye zizi la mbuziiiiii,
CHORUS
Kwa kinywa chako ulisema unanipenda unanithaminiiiiii,
Ona sasa umeumbuka na umefanya niniiiiii,
Hii jeans ya naniiii? ahaaaa,
Hii shati ya naniiii?
Hii buti ya naniiiiii? ahaaaa,
Na hii simu ya naniiii?
VERSE-2
Haya sasa chagua nikupe adhabu ganiiii, ohoooo
hakuna forgiveness huruma wala niniiii, heieiei
Haya sasa chagua nikupe adhabu ganiiii, ohoooo
hakuna forgiveness huruma wala niniiii, heieiei
Sielewi ni tamaa zako tuu au tabia,
Umeshindwa kuniheshimu wanaume hadi ndani unaletaaaa,
Za mwizi arobainiii,
Leo hii utanieleza niniiii.
CHORUS
Kwa kinywa chako ulisema unanipenda unanithaminiiiiii,
Ona sasa umeumbuka na umefanya niniiiiii,
Hii jeans ya naniiii? ahaaaa,
Hii shati ya naniiii?
Hii buti ya naniiiiii? ahaaaa,
Na hii simu ya naniiii?
VERSE-3
Na kudadeki huyu aliemo humu ndani ama zangu ama zake,
Haiwezekani ndani kwangu ageuze kama kwake,
Na kudadeki huyu aliemo humu ndani ama zangu ama zake,
Haiwezekani ndani kwangu ageuze kama kwake,
Atanieleza "ohooo",
Atanitambuaaaaa, "ahaaa"
Atanijua "eheee"
Atanisoma ahaaa
CHORUS
Kwa kinywa chako ulisema unanipenda unanithaminiiiiii,
Ona sasa umeumbuka na umefanya niniiiiii,
Hii jeans ya naniiii? ahaaaa,
Hii shati ya naniiii?
Hii buti ya naniiiiii? ahaaaa,
Na hii simu ya naniiii?
Friday, February 26, 2010
HUSSEN MACHOZI AACHIA WIMBO MPYA ZA MWIZI 40
Friday, February 26, 2010
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Comments:
Post a Comment