Monday, January 11, 2010

Nina mpango wa kufungua kampuni yangu ya ulinzi-jaguar

Msanii wa muziki wa hip hop nchini Kenya, Jaguar amesema kuwa mwaka huu wa 2010 ni mwaka wa kupambana na kila hali kuhusiana na muziki na pia ana mpango wa kufungua kampuni yake ya ulinzi nchini humo kwa kuwaajiri wakenya.

Jaguar amesema kuwa bidii yake katika muziki ndiyo itakayomnyajua juu, kwa sasa msanii huyo anayetamba na kibao chake cha nimetoka mbali alichoshikiana na Ay ambacho bado kinaendelea kusumbua katika anga ya muziki Afrika mashariki.

Msanii huyo ambaye anamiliki magari ya teksi nchini humo na pia ni msanii anayejituma sana katika kufanikisha muziki wake unafika katika levo ya kimataifa.

0 Comments: