Athur,DNA na Langa
Moja ya kipande cha nyimbo yake ya Banjuka
Natumai mashabiki na wapenzi wa msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Kenya aliyetamba na kibao chake cha banjuka, DNA kuachana na muziki wa kidunia na kujiunga na nyimbo za dini,ni umaarufu huu uliopelekea wimbo wake huo kutumiwa na wanasiasa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
DNA ambaye ni (Dennis Kaggia) kwa sasa amechukua mwelekeo mpya baada ya kuokoka, na hii hapa ilikuwa ni “Interview” aliyofanya moja kwa moja na safu hii kuhusiana na kugeukia nyimbo za dini.
Swali:Wewe ni mmoja wa wasanii waliokuwa wakivuma mno hasa katika muziki wa kizazi kipya.Mbona umegeukia injili?
Jibu:Hizi zilikuwa ni sifa za kidunai tu,sasa ninalenga zaidi sifa za mbinguni.nilifunguliwa macho ya ndani na kutambua kwamba nilikuwa nimepotoka kwa kiasi fulani.baada ya kufunuliwa njia iliyo ya kweli,nimeamua kuifuata na ndipo sasa ninaeneza injili kupitia nyimbo zangu za sasa.
Swali:Unamaanisha nini unaposema kwamba ulikuwa umepotoka? Kwani kuimba muziki wa kiburudani ni kupotoka?
Jibu:Muziki wa burudani si kupotoka hata kidogo ila mambo yanayotendeka huko ndiyo mabaya zaidi.Katika hali ya kujitafutia umaarufu,wasanii wengi wanajuhusisha katika visa vya kusikitisha mno kama vile matumizi ya dawa za kulevya ,kulewa ovyo,uvutaji wa sigara na hata bangi na kwenda na wanawake tofauti kama njia ya kujitafutia umaarufu.
Swali:Hivyo na wewe ulishafanya kabla ya kuokoka?
Jibu:Ndio nilitumia dawa za kulevya na vileo vingine vya aina mbalimbali ambavyo viliniathiri sana ila namshukuru Mungu kwa kuniepusha navyo kabla ya havijanidhuru.kwa hakika nilifika mahali hata nikapoteza hamu ya kula chakula na nilipungua uzito wangu kwa kiasi kikubwa mno.
Swali: Pole sana ,Kitu gani ulichoamua baada ya hapo?
Jibu:Ilinibidi nitafute ushauri nasaha kwenye kituo maalum kuhusu namna ya kuepuka matumizi ya dawa za kulevya.Hii ndio sababau ya kutoweka kwenye burudani kwa miezi kadhaa na wale mashabiki wangu wanaofuatilia muziki wangu watambue hilo na sikuonekana mahali popote.
Swali:Unajihisi umebadilisha maisha yako hivi kwamba hautaathirika na ulevi?
Jibu:Nimebadilika kabisa sio kidogo na sasa nimeingia kwenye nyimbo za injili kwa ukamilifu wa hali ya juu.Wale wenye hamu na nyimbo zangu za dini watanikubali kwa hilo wenyewe.
Swali:Kwa hiyo unarekodia wapi nyimbo zako za dini na je,umebadilisha wasimamizi wa muziki wako?
Jibu: Kwa sasa nimehamia katika studio ya Jomino Entertainment na nimejiunga na kampuni ya The Rainmaker ambapo meneja wangu ni Simon Wainaina.Yeye ndio anawasimamia waimbaji wengine maarufu kama vile Eric Wainaina ambaye ni nduguye ,Suzzana Owiyo miongoni mwa wengine wengi ambao haitakuwa kusara kuwataja bila idhini yao.
Swali:Kuna uwezekana wa kubadilisha jina lako la DNA kwani litakuwa linaendana bado na muziki wa kidunia.?
Jibu:Kwa hilo halina haja, Hili ni jina tu la kisanii na wala si la ubatizo .Muhimu ni yale matendo yaliyomo moyoni mwangu kama mwimbaji wa injili.
Swali:Wasani wengi waliwahi kung’atuka kutoka kwenye burudani na kujiunga na injili ila mienendo yao ilianza kutiliwa shaka aiendani na mambo ya mungu.Unadhani Sababu ni nini?
Jibu:Sitaki kuzungumza kwa niaba ya mtu mwingine.Hata hivyo ninachofahamu ni kwamba ,uamuzi hutoka moyoni tu.Iwapo mtu amechukua nafasi ya kuzungumza na mungu wake,sidhani kama anaweza akarejea tena kwenye mambo ya kidunia baada ya muda.Hata hivyo,siwalaumu kwa maana wengine wanakuwa na sababu zao ikiwa ni pamoja na aina ya marafiki wanaokuzunguka.
SWALI:Kwa hiyo una mpango upi kwa sasa kimuziki.
Jibu:Ninaishughulikia albamu yangu ya injili ambayo itazinduliwa baadaye mwaka huu.
Monday, January 18, 2010
Najiona niko tofauti kuimba nyimbo za injili-DNA!
Monday, January 18, 2010
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Comments:
Post a Comment