Msanii wa kizazi kipya ambaye ni chipukizi kutoka mkoani Mwanza, SAJNA amekuja na kibao chake kipya kinachokwenda kwa NADHIFA ambacho kinazungumzia stori ya kweli.
Akichonga na kona hii msanii huyo ambaye anatoka lebo ya Tetemesha Recordz na kazi imefanywa na A2P RECORZ chini ya produza SAM TIMBER ili kumtambulisha kijana huyo kwa mwaka huu wa 2010 ambaye ni kijana wa miaka 18,aliyezalimia kuwafunika wakongwe wa muziki hapa nchini.
“Ninawaomba mashabiki wangu wanipokee kwa mikono mwili ili niwaonyeshe mabo mapya kutoka kwangu kwa mwaka huu wa 2010 na nimezamila kufanya kweli katika anga ya muziki hapa Bongo na Afrika Mashabiki kwa ujumla, “alisema Nadhifa.
SAJNA alisema wimbo huo ni stori ya kwli ambayo imemtokea yeye mwenyewe, na kila alichokiimba katika wimbo huo ni cha kweli kinachomhusu yeye na familia yake na pia amemuimba dada yake wa damu ambaye alitoweka nyumbani kwao bila taarifa miaka kadhaa iliyopita.
Monday, January 4, 2010
Mwaka mpya SAJNA kuwashika wakongwe
Monday, January 04, 2010
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)






0 Comments:
Post a Comment