Ebwana eh! Dj Choka aliyekuwa akifanya kazi na Zizzou Entertainment habari zimetufikia amejiachia katika umoja huo na kuendelea na mambo yake kama kawaida ila mpaka sasa haijulikani ni nini kilichomtoa katika umoja huo.
Kabla ya hapo Dj Choka alikuwa akifanya kazi na Zizzou Entertainment kama dj wa umoja huo ambao ulikuwa na wasanii kama vile Mr Blue, Ngwair, Steve, baby Boy na Sqeezer.
Ila tutamsaka na kujua kilichomtoa Zizzou Entertainment ni masilahi au kuna kingine ambacho mashabiki wake wajue kwani kabla ya hapo alikuwa na Prof jay ila napo alijiachia na kuwa kivyake.
Kwa hili hatujui ni nini?
Tuesday, January 19, 2010
Dj Choka ajiachia Zizzou Entertainment
Tuesday, January 19, 2010
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Comments:
Post a Comment