Friday, January 22, 2010

Blu 3 wanataka kuachana?

Nakaaya, Mwana FA na Blu3
Kuna nyepesi nyepesi zimetufikia ya kwamba wanadada watu wanaounda kundi la Blu 3’ wanataka kuachana. Habari hizo zinasema kuwa wanadada hao wanataka kumfuata mwanachama mwenzao aliyejiengua katika kundi hilo “Cindy” ili kufanya nae kazi.

Kundi hilo la Blu 3 lililoanzishwa mwaka 2004 ambapo kwa sasa linaundwa na wanadada Jackie, Mya na Lillian. Wanadada hao mpaka sasa wana albamu tatu walizorekodi wao.

Tulimtafuta Jackie kuongea nae juu ya tetesi hizo lakini hakupatikana kwa njia ya simu ila tutamtafuta ili kuliongolea suala hilo kama lina ukweli wowote ndani yake.

0 Comments: