Tuesday, August 29, 2017

Ommy Dimpoz afuta picha ya mama Diamond

HATIMAYE msanii Ommy Dimpoz ameamua kufuta posti aliyokuwa ameiweka mtandaoni huku ikiwa imeambatana na picha ya mama yake Diamond.Wiki hii kwenye mitandao ya kijamii moja ya gumzo ambalo limeendelea kuwepo ni malumbano ambayo yanaendelea kati ya Dimpoz, Diamond na Ali Kiba.

Hata hivyo Dimpoz aliamua kuandika ujumbe na kisha kuweka na picha ya mama yake Diamond hali ambayo imekasirishwa watu wengi na kumuonya aache kufanya hivyo.Ndio maana ameamua kuitoa.
Meneja wa zamani wa Ommy Dimpoz Mubenga, Aunty Ezekiel na hata Dada wa Diamond wameonesha kusikitishwa na kitendo hicho na kuwamba wasanii kuacha tabia ya kuingiza wazazi kwenye malumbano yao.

0 Comments: