Tuesday, August 1, 2017

Ndoa sasa yaanza kunukia kwa Shilole

MSANII Zuwena a.k.a Shilole amedai tayari ameshatolewa barua na mpenzi ambaye amekuwa naye kwenye uhusiano kimapenzi na Mungu akimjalia atafunga naye ndoa ili kuhalalisha.
Ametoa kauli hiyo wiki hii na kusisitiza ameamua kuweka uhusiano wake faragha kidogo ili awe huru na mpenzi wake.
“Kwa sasa hivi sina boyfriend kabisa ila nina mchumba na ameshanitolea barua.Mungu akipenda nitafunga naye ndoa siku si nyingi kuanzia sasa,’anasema.
Kuhusu wapenzi waliopita kuwa na uhusiano na marafiki zake anasema anaona ni kitu cha kawaida kwa sababu anaamini mapenzi ni kama daladala mmoja akishuka , mwingine anakaa.

0 Comments: