Wednesday, August 16, 2017

Lulu Diva ajivunia uzuri wake

STAA Lulu Diva ameamua kujimwagia sifa kuwa yeye ni mzuri na ndivyo anavyoamini yeye na hata mama yake ambaye tangu akiwa mdogo amekuwa akimsifu kwa uzuri alionao.
Lulu anaendelea kueleza kuwa yeye ni msichana ambaye anamvuto na mama yake alikuwa akimwambia “Lulu mwanangu mashallah, yaani hapa sidhani kama kuna mtu nitamwambia idadi ya ngíombe ninazozitaka halafu akapindua.”
Anasema kwa kuwa alijitambua mapema kuwa ni mzuri hiyo imemsaidia kutorubunika na hata akitokea mtu akamwambia kuwa ni mzuri anaona ni jambo la kawaida kwake.
“Nilijijua na naendelea kujijua kuwa mimi ni mzuri, asitokee mtu akanisifu kwa uzuri niliona nao halafu anidanganye kwa chips kuku huyo atakuwa anajisumbua,”anasema Lulu.

0 Comments: