Tuesday, August 22, 2017

Kim Kardashian aajiandaa kupata mtoto

MWANAMUZIKI Kim Kardashian amethibitisha kuwa yeye na mumewe Kanye West wanatarajia kupata mtoto mwingine kutoka kwa mwanamke ambaye anadaiwa wamemlipa ili abebe ujauzito huo.
Amethibitisha hilo kupitia jarida la The Hollywood Reporter lillilotoka wiki hii ambapo familia ya Kardashian imefanikiwa kukava kwenye jarida hilo.
Mwanamuziki huyo anafafanua kuwa kumekuwa na mambo mengi yanasemwa kuhusu yeye na mumewe lakini hawakutaka kuthibitisha chochote .” Hakika sisi tumejaribu. Tunatarajia hivyo,î anasema Kim.
Kim na Kanye wanadaiwa kuwa wamemlipa mwanamke huyo zaidi ya dola 4500 kwa ajili ya kubebea mimba itakayowaletea mtoto wa tatu atakayezaliwa Januari mwakani.

0 Comments: