Tuesday, August 22, 2017

Chris Brown ajuta kumpa kipigo Rihanna


MSANII maarufu nchini Marekani Chris Brown ameamua kueleza sababu ambazo zilimfanya aachane na mpenzi wake Rihanna baada ya kumtwanga ngumi za kutosha.
Anaeleza hayo ikiwa ni miaka nane imepita sasa tangu wawili hao kuachana  ambapo kupitia documentary yake ya Welcome to My Life’, Chris anaonesha kusikitishwa na kitendo cha kumpiga na kumuumiza Rihanna.
Anasema Rihanna alificha funguo ya gari na kusema imepotea na wakatoka nje kuitafuta ndipo mwana dada huyo akaanza kupiga kelele za msaada akidai Chris anataka kumuua.Hata hivyo Chris anapinga vikali madai hayo.
Baada ya hapo Chris alijikuta kifungo cha uangalizi wa miaka mitano kwa shabulio hilo na siku 180 za adhabu ya kufanya kazi za kijamii na mwaka mmoja wa ushauri nasaha.Hivyo kupitia documentary hiyo ameeleza kwa kina historia ya maisha yake.

0 Comments: