Saturday, July 22, 2017

Unene wamchosha Aunt Ezekiel

MUIGIZAJI wa Bongo Muvi Aunt Ezekiel ameamua  kusafiri kwenda Thailand kwa ajili ya kutafuta dawa ya kupunguza unene baada ya kuona hali hiyo inamnyima raha.
Aunt Ezekiel anasema wiki hii kuwa baada ya kufanya kila jitihada za kupunguza unene na kuona hapungi aliamua kufunga safari hadi nchini Thailand kwa ajili ya kutafuta dawa na baada ya kuitumia anakiri kuna mabadiliko anayaona.
Anafafanua kutokana na unene aliokuwa nao ilifika hatua  hata akivaa nguo nzuri alikuwa hapendezi na baada ya  kuanza kutumia dawa hiyo anaona kuna mabadiliko makubwa.

0 Comments: