MWANADADA ambaye anatesa kwenye Bongo Fleva Shilole amewataka vijana wa mjini ambao wanachukua ‘Account’ za watu mitandaoni waende kuiba kwenye taasisi za fedha na si kwenye mitandao ya jamii kwa kuwa huko hakuna fedha.
Akizungumza wiki hii Shilole anasema icha ya ‘mwizi wake’ kumuachia akaunti yake ya Instgram lakini anataka mtu huyo apatikane na ikiwezekana afungwe jela iwe fundisho kwa wengine wanaojihusisha na michezo hiyo kwani wamekuwa wakiwakwamisha na kuwarudisha nyuma wasanii.
“Akaunti yangu kuna mtu aliingilia lakini nashukuru Mungu kwasasa ipo kwenye mikono yangu lakini hao vijana wanaojifanya wao wamesomea IT na kuanza kuiba akaunti za watu za mitandao ya jamii, wakaibe benki,”anasema.
Anafafanua kitendo cha akaunti yake kuingiliwa na wezi imemuingizia hasara kwani ameshindwa kutoa wimbo wake mpya na ameshindwa kutangaza kuhusu biashara yake ya chakula.
“Hawa watu wanaoingilia akaunti zetu za mitandaoni wanatutia hasara na kutuharibia malengo yetu kwenye masuala ya muziki. Instgram inanisaidia kutangaza muziki wangu, inanisaidia kutangaza biashara yangu ya chakula na mambo yangu mengi na yote yalikwama kwa zaidi ya mwezi mmoja,”anasisitiza.

0 Comments:
Post a Comment