Tuesday, August 1, 2017

Safaree atamani Nicki amzalie mtoto

KWA mara nyingine tena Rapa Safaree ameamua kutuma ujumbe kwa aliyekuwa mpenzi wake kwa miaka 12 Nicki Minaji kuwa anatamani amzalie mtoto.
Kupitia mtandao wa Twitter, Safaree amemwambia Nicki kuwa anahitaji kupata mtoto kutoka kwake.”Nicki nahitaji kupata mtoto kutoka kwako, naomba unizalie mtoto,”ameandika msanii huyo.
Unapofuatilia post nyingi za Safaree utabaini kuwa bado anampenda aliyekuwa mpenzi wake na anaumia kumpoteza.Hata hivyo kwa Nicki anaonekana kutogeuka nyuma na sasa anaendelea kula bata akiwa na Meek Mill.

0 Comments: