Msanii wa Pop Lana Del Rey ameachia nyimbo mpya mbili akiwa amemshirikisha msanii A$AP Rocky ikiwa ni maandalizi ya albamu yake ya Lust for Life ambayo amepanga kuitoa Julai 21,2017.
Lana ameachia nyimbo zake hizo mpya mbili ambayo ni “Groupie Love” akiwa amemshirikisha rapa A$AP Rocky, na “Summer Bummer,” akimshirikisha A$AP Rocky na Playboi Carti.
Lana ni chimbuko jipya la wasanii wa pop wanaokuja kwa sasa katika ulimwengu wa muziki duniani.
albamu ya Lust for Life ya Lana’s itakuwa na nyimbo tano pia amewashirikisha wasanii kama vile Sean Lennon na Stevie Nicks.
0 Comments:
Post a Comment