Saturday, July 1, 2017

Ndoa yamfanya Shamsa afunge Ramadhan kihalali

MWIGIZAJI wa filamu za kibongo Shamsa Ford amesema mfungo wa Mwezi wa Ramadhani ambao tayari umemalizika ndio ulikuwa wa halali ukilinganisha na mingine ambayo imepita kwani mwaka huu amefunga akiwa ndani ya ndoa.
Shamsa anasema Ramadhan ya mwaka huu ameifunga kihalali , tofauti na miaka iliyopita ambayo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume Mkristo ambaye wakati mwingine alitaka kuwa naye bila kujali mfungo.
“Namshukuru Mungu kwani mwaka huu nimefunga na kumaliza Ramadhani kihalali maana niko ndani ya ndoa si kama miaka iliyopita nilikuwa nafunga kama mchezo, kiukweli najivunia sana kumaliza salama mwezi huu,”anasema.

0 Comments: