Tuesday, July 25, 2017

Mchekeshaji Mzee Majuto hajafa


Comedian Mzee Majuto is not dead!

Kama utakuwa mpenzi wa vichekesho vya Swahili basi naamini kabisa watakuwa sio jina geni la  Mzee Majuto!
Kabisa, Mzee Majuto ni mmoja wa wasanii vipenzi wa vichekesho kutoka Tanzania ambaye yupo katika vichekesho kwa miaka mingi mpaka sasa. Na pia ameshacheza katika baadhi ya nyimbo za wasanii mbalimbali wa muziki wa bongo fleva kama muhusika!


Mzee Majuto
Bila shaka siku chache zilizopita kuna uvumi ulienea katika mitandao ya kijamii ikisema msanii huyo wa vichekesho amefariki. Mmoja wa marafiki wake wa karibu alikuja na kusema huo unaonea katika mitandao ya kijamii ni uzushi mtupu kwani mzee majuto anaendelea vizuri kwani kweli alikuwa anaumwa ila ni kutokana na umri wake.
Kupitia mtandao wa jamii wa page yake ya Instagram Haji Salum kwa jina maarufu Mboto aliandika na kusema;


Mzee Majuto’s hali yake kiafya
“Baada ya kupata taarifa mbaya kuhusu Mzee Majuto nimelazimika kuja kwake Tanga. Ni kweli anaumwa ila anaendelea vizuri na si kama watu walivyozusha kuwa mzee hatunaye. Kwa sasa mzee ni mzima nipo naye Tanga,”


0 Comments: