KUMEIBUKA madai kuwa wakati ikiwa ni siku kadhaa sasa tangu aliyekuwa mumewe, Ivan Ssemwaga ‘Ivan Don’ azikwe nchini Uganda baada ya kufariki dunia , Zarinah Hassan ‘Zaribosslady’ anadaiwa kuwatibua Waganda kutokana na baadhi ya mambo anayofanya kwa madai yanatia aibu.
Baadhi ya vyombo vya habari vya udaku nchini Uganda, tofauti na ilivyotarajiwa, kama ilivyo kwa baadhi ya tamaduni za Kiafrika, kuwa Zari angekuwa kwenye maombolezo kwa siku arobaini au hadi amalize eda kwa kufiwa na mume huyo, yeye amekuwa akijihusisha na ishu ambazo zinaacha watu midomo wazi.
Kwa mujibu wa vyombo hivyo vimetoa orodha ya mambo kadhaa ambayo wanadai ndio yanayomfanya Zari aonekane ni kituko na kuitia aibu kwa Waganda.Baadhi ya mambo hayo inadaiwa siku mbili baada ya mazishi ya Ivan Zari alitupia video kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii ikimuonesha mwenye furaha tele.
Wakati aibu nyingine ni ni pale alipotaka kuzichapa kavukavu na binamu wa Ivan, King Lawrence kwenye kikao cha familia ya jamaa huyo kilichomuhusisha Zari juu ya usimamizi wa mali za baba watoto wake huyo.
0 Comments:
Post a Comment