LEO katika Zeze Kolabo ninakuletea ‘pea’ ya wasanii ambao kama wangefanya kolabo kwa mwaka huu au miaka ijayo, basi kolabo hizo zingeandika historia nyingine katika muziki wa Bongo Fleva, na hata kuvunja rekodi, twende sawa.
Davido, Joh Makini
Davido kutoka nchini Nigeria alipata umaarufu mkubwa nchini mara baada ya kufanya kolabo na Diamond Platnumz ikiwa ni remix ya wimbo wa My Number One.
Mapema mwaka huu Joh Makini kutoka kundi la Weusi alionyeha picha akiwa nchini Afrika Kusini ambapo walikuwa wanakamilisha kutengeneza video ya wimbo wao, hata hivyo Joh Makini aliporejea nchini hakuweka wazi ni lini wimbo huo utatoka ila alisema kazi hiyo imeshakamilika.
Joh Makini ameshafanya kazi na msanii wa Nigeria ambaye ni Chidenma katika wimbo wake Perfect Combo iliyotoka mwaka jana na kufanya vizuri.
Mwana FA, Lady Jaydee
Miongoni mwa wasanii wambao walishafanya kolabo nyingi kipindi cha nyuma na kufanya vizuri ni Mwana FA na Lady Jaydee.
Walishafanya kolabo ambazo zilisumbua katika bongo fleva na hadi leo hii zikipingwa watu wanasimama na kucheza na kurudisha kumbukumbu zao nyuma.
Unakumbuka nyimbo kama Wanaume kama mabinti, Hawajui, Msiache kuongea na Alikufa kwa ngoma, hiyo ni historia waliyoiandika pamoja.
Miaka kama minne nyuma kuliripotiwa kutoelewana baina yao, na hadi leo hii ukimya umetawala na hakuna chochote kinachoendelea kati yao.
Mwishoni mwa mwaka jana Lady Jaydee aliiambia Citizen Radio ya Kenya kuwa anakipindi kirefu hajawasilina na Mwana FA kutokana na baadhi ya mambo kutokaa sawa kati yao, tuanchane na hilo.
Vanessa Mdee, Mimi Mars
Vanessa Mdee akiwa na miaka kadhaa katika muziki wa Bongo Fleva, mgogo wake Mimi Mars mwaka jana ndio amenza na hadi sasa ana nyimbo mbili (Sugar, na Dedee).
Hivi majuzi amekaririwa akisema hawezi hafikirii kufanya kolabo na Vanessa kama sehemu ya yeye kujitangaza bali anataka kupambana pekee yake. Mashabiki wao wanangojea kama kauli hiyo itakuwa na ukweli ndani yake.
Diamond Platnumz, Alikiba
Kwa sasa ni kama muziki wa Bongo Fleva upo mikononi mwao, muziki wao unatoa picha halisi ya kule Bongo Fleva inapoelekea kufikia mafanikio makubwa zaidi.
Ushindani wao umeichangamsha Bongo Fleva na hadi sasa inaonekana kuwa ni biashara kubwa ambayo inaweza kuajiri kundi kubwa la watu.
Si kwenye jukwaa tu ndio wanakuwa washindani bali hata nje ya muziki huo, mashabiki wao na vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kutoelewana ingawa hakuna anayeweza kudhibitisha hilo.
Mwaka jana Alikiba alilalamikia kitendo cha yeye kuzimiwa maiki alipokuwa akifanya ‘show’ Mombasa Kenya na kuhusisha tukio hilo na meneja wa Diamond Sallam aliyeonekana maeneo hayo.
Matukio kama haya na yale ya kuwa na timu kwenye mitandao ya kijamii ndio yanafanya ushindani wao kuwa mkubwa.
Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye aliwahi kukaririwa akisema hapendezwi na vuta ni kuvute za wawili hawa, na wengine wakaenda mbali zaidi wakisema watoe nyimbo pamoja ili kukata mzizi huo wa fitina.
Lakini wataalamu wa muziki wanaonya kufanya hivyo kutaondoa ushindani na hata ile biashara wanayofanya huenda ikashuka, ingawa mashabiki wanaomba hilo kutokea.
Hata mwaka huu walipotakiwa kukaa pamoja na kutoa wimbo kwa ajili kuhasisha watu kuichingia timu ya Taifa chini ya 17 ‘Serengeti Boys’, hilo lilishindikana. Hata Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe aliposhauri wafanye hivyo, bado ilishindikana.
Joh Makini, Fid Q
Ukizungumzia muziki wa hip hop kwa sasa hapa Bongo huwezi kuacha kutaja hivi ‘vichwa’ vinavyosifika kwa uandishi na kurap pia.
Ni muda mrefu mashabiki wamekuwa wakiwalinganisha katika ngoma zao, huku wao wakijibizana kwenye mistari, uzuri wao ni kwamba wanaelewana vizuri ila mistari yao ndio haitaki kukaa katika nyimbo moja.
Prodyuza kutoka MJ Records Marco Chali aliwahi kukaririwa akisema moja ya vitu angependa kuviona katika Bongo Fleva, ni kolabo ya wawili hawa.
Si Marco Chali tu, bali kila shabiki anatamani kuona hilo linafanyika, swali ni je, ni lini na wapi?, tuwaachie wao.
Peter Akaro
Kwa maoni 0755 299596

0 Comments:
Post a Comment