Monday, May 8, 2017

Unaambiwa Ritha anaogopa wanaume balaa


RITHA Silvanus amesema kuwa sababu pekee ya yeye kutojiingiza kwenye mahusiano ni wanaume aliokuwa nao mwanzoni kutokuwa waaminifu na hivyo kujawa hofu dhidi yao.
“Wanaume ndio waliuvunja moyo wangu na wala sio kwamba sipendi kuwa na mpenzi, nimeteseka sana na mapenzi na kote nilipopita sikuwahi kupata muaminifu ambaye hakuniumiza, sijui kwanini hawaridhiki,” alihoji Ritha.Staa huyo amesema kwenye maisha yake amekuwa akiogopa kukurupuka kuingia kwenye mahusiano na mwanaume bila kumchunguza kwakuwa anaogopa kuumia kwa jambo ambalo angeweza kuliepuka.


0 Comments: