Thursday, May 11, 2017

Sean Combs aongoza jarida la Forbes kuwa rapa tajiri duniani





Miaka saba sasa mwanamuziki nguli duniani, Sean Combs ametwajwa na jarida la  tops Forbes kwenye listi tano bora ya mwanamuziki rapa tajiri duniani.

Mwanamuziki huyo ambaye ana miaka 47 ni baba wa watoto watano anayekadiliwa kuwa na utajiri wa kiasi cha dola milioni  $820, shukrani wake kwa uwekezaji kubwa anaoufanya.

Msanii Combs ambaye anamiliki Revolt TV, vinjwaji kama Ciroc Vodka  na maji ambayo inayomfanya kumpandisha chati kila mwaka.

Rapa nguli  Jay Z nae anamfuata msanii Combs kwa ukaribu ambaye nae anakadiliwa kuwa na utajiri wa dola milioni  $810. Jay Z ambaye jina lake kamili ni Shawn Carter, mwenye umri wa miaka 47, anayemiliki mtandao wa kuuza muziki wa Tidal, kampuni ya muziki ya burudani ya Roc Nation pamoja na shampeni ya Armand de Brignac.

Msanii Dr. Dre yeye anashika nafasi ya tatu akikadiliwa na utajiri wa dola milioni  $740 huku akifuatwa nyuma na msanii na mmiliki wa Young Money  Bryan ‘Birdman’ Williams ambaye ana utajiri wa dola milioni  $110 million.

Msanii ambaye ni mkanada Drake naye yupo namba tano mwenye utajiri wa dola milioni  $90.

0 Comments: