Tuesday, May 16, 2017

Harmorapa amtunishia msuli Afande Sele


WIKI iliyopita Mfalme wa Rhymes nchini Tanzania, Afande Sele amezungumzia hali ya muziki ilivyo kwa sasa na kwenye mazungumzo hayo huku akisema hajui ngoma yoyote ya Harmorapa.
Akaongeza hata kwa mara ya kwanza kumuona ni pale alipotokea kwenye tukio la Nape Nnauye aliposhikiwa bastola, hivyo haelewi muziki anaoufanya zaidi ya kumuona mitandaoni tu.
Hatimaye Harmorapa amemjibu Afande Sele kwa kueleza wiki hii kuwa hana muda wa kujibizana na mtu bali anaacha kazi zake ndiyo zimjibu na kusisitiza hakuna msanii aliyeanzia juu kwani hata yeye(Afande Sele), alianza chini.
“Nieleze tu yeye kwanza mwenyewe akae chini na kujua na kukumbuka kuwa alianzia chini mpaka kufika kiwango fulani watu wakamkubali,”anaendelea kumuonya Afande Sele kuwa “ Ajue mimi kama Harmorapa sina maneno mengi ila kazi zangu ndiyo zitakuja kumuelekeza kuwa Harmorapa uliyekuwa unamuongelea ndiyo huyu kupitia kazi yangu ndiyo itakuwa imemnyoosha au vipi? na  ku’prove ukali wa Harmorapa.”


0 Comments: