STAA wa video za muziki na hasa wa kizazi kipya Gigy Money ameendelea kuchafua hali ya hewa na safari hii amemchana kipenzi cha Watanzania walio wengi Wema Sepetu anaishi maisha ya kuigiza kila kukicha.
Gigy amedai japo mwanzoni alitamani kuwa kama Wema na kukiri kuwa alishawahi kutamani kuwa wa mtu wa mfano kwake lakini kwa sasa hataki tena.
“Wema ni mtu kupenda kuigiza, ukimuona Wema hivi ‘live’ na ukimuona mtandaoni unaweza ukavurugwa, watu wengi ambao hawajawahi kumuona Wema hivi live wanachanganyikiwa.
“Si kama mimi sasa hivi. Nilikuwa navurugwa magazeti kila siku nikiensda shule napitia Wema kafanya nini? Sasa hivi naishi hayo maisha sasa huwezi kuniambia,”anasema Gigy.
Anaongeza “Naishi hayo maisha ‘by real’ sasa ndio maana kwake inakuwa changamoto, atafanya nini. Mimi ni changamoto kubwa sana kwa kila mtu ambaye yupo kwenye industry hii.
“Maana sasa hivi unaweza ukaenda kwenye ‘interview’ ukamfanyia msichana ghafla akamtaja Gigy from nowhere pia. Mimi sifanyi kwaajili nashindana, nafanya kwa ajili yangu.”
Anasisitiza ni kweli zamani alikuwa atamani kuwa kama Wema katika mambo ya filamu , kwani aliamini Wema ni msichana mzuri hakuna.
Kuhusu kukutana na Wema, Gigy anasema “Mara mwisho nilipokutana naye alikuwa ameninunia na alikuwa ananiangalia vibaya,”.

0 Comments:
Post a Comment