Saturday, May 27, 2017

Emmanuel Mbasha adai hana mpango wa kuoa


MWIMBAJI wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha amesema hafikirii kufunga ndoa kwa haraka ili awe na mke.
Mbasha ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tu aliyekuwa mkewe Frola Mbasha kufunga ndoa na mwanaume mwingine.
Anasema  changamoto kubwa aliyoipata katika ndoa imemfanya kila mwanamke anayemuona anamuogopa kwani ameshaumizwa , hivyo nguvu na akili yake ameiweka zaidi katika kufanya kazi zake binafsi.
“Sina wazo la kutaka kuwa na mke na unajua ukishakutwa na jambo basi hofu inakuwa kubwa.Nipo naendelea na kazi zangu na nina muomba Mungu anijaalie katika maisha yangu na kuniongoza kwa kila ambalo nalifanya,”anasema.


0 Comments: