Wednesday, May 17, 2017

Ujumbe wa Zari wazua gumzo mitandaoni


http://www.ghafla.com/ke/wp-content/uploads/sites/4/2017/05/Ivan-sick.jpg


UJUMBE wa mwanamama ambaye kwa sasa ni mzazi mwenzake staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinum, Zari Hassan umezua tafrani kwenye mitandao ya kijamii.

Ujmbe huo ambao mama Tiffa aliupost Jumatatu, ulisomeka “These two days have been difficult for me. Let us pray for Ivan” ukiwa na maana sawa na ‘Siku mbili hizi zimekuwa ngumu kwangu. Sote tumuombee Ivan’ umegeuka kuwa gumzo licha ya mwenyewe kuupost kwa nia njema.
Gumzo hilo linakuja katika kipindi ambacho aliyekuwa mumewe Zari, Ivan Ssemwanga alikutwa akiwa hajitambui na kulazimika kukimbizwa hospitali ya
Steve Biko, Pretoria nchini Afrika Kusini.

Baadhi ya wachangiaji walijikuta wakizozana kutokana na wengine kudai kuwa, ujumbe wake ni dharau kubwa kwa supastaa wa Tanzania, Diamond.
“Kusema kuwa siku mbili hizi zimekuwa ngumu kwake, ni dharau kwa Diamond ambaye kwa sasa yuko naye” alisema mchangiaji mmoja.
Mchangiaji mwingine alisema ujumbe wa kumwombea mzazi mwenzake wa zamani si mbaya, ila ubaya unakuja pale Zari anaposema kuwa siku hizo zimekuwa ngumu kwake.
“Ameonesha kumjali mzazi mwenzake huyo wa zamani, lakini kaenda mbali zaidi alipodai kuwa siku hizo zimekuwa ngumu kwake” alisema mchangiaji huyo.
Hata hivyo, wachangiaji wengine walisema kuwa ujumbe huo ni muhimu kwani unaonesha utu na namna mwanamama huyo alivyo makini hasa linapokuja suala muhimu la afya ya mzazi mwenzake huyo.
Mbali na kuandika ujumbe huo, Zari pia aliambatanisha picha yake alipomtembelea Ivan hospitalini hapo alikokuwa akipatiwa matibabu.

0 Comments: