Saturday, April 22, 2017

‘Rangi ya ngozi ilininyima usingizi utotoni’

STAA wa filamu nchini Afrika Kusini, Pearl Thusi ameweka hadharani namna ambavyo alikuwa akitamani kuwa na rangi nyeusi enzi za utotoni.
Pearl amesema ilimlazimu kukaa juani kwa muda mrefu ili kuweza kubadili rangi ya mwili wake kutoka kuwa mweupe ili iwe nyeusi akiamini kuwa mweusi kungemuongezea urembo zaidi, jambo ambalo liliwafanya wanafunzi wenzake shuleni kumcheka.

“ Kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwangu nilitamani kuwa na rangi nyeusi nikiamini ingeongeza urembo wangu jambo ambalo lilikuwa likinisababishia kuumia kwa kukaa muda mrefu juani, lakini nashukuru wazazi wangu kwa kunijenga kisaikolojia na leo naipenda ngozi yangu,” anasema Pearl.


0 Comments: