Saturday, April 22, 2017

Mrembo Ellen azidi kukata mawimbi


KUPANGA ni kuchagua, ndivyo hali inavyojionesha kutoka kwa mrembo Ellen Kyei ambaye ameamua kuacha kuigiza filamu zinazotayarishwa na wenzake na sasa ameamua kuvaa jukumu la kuandaa, kucheza kazi zake mwenyewe.

Ipo hivi, baada ya kufanikiwa kuachia filamu tatu chini ya utayarishaji wake mwenyewe, Ellen sasa amejipanga kutoa chuma cha nne ambacho amekipa jina la ‘The List’.
“ Unapoamua kufanya kazi zako mwenyewe ujue utakutana na changamoto nyingi lakini hapo ndio mafanikio yalipo, nimekomaa na sasa natoa fialmu yangu ya nne ambayo wakali kibao akiwemo, Ellen White, Mama Cali na Funny Ley,” anasema Ellen.



0 Comments: