Saturday, April 29, 2017

Kwaku amtaja staa anaemkubali


MAISHA ni kukubali kile ambacho kinafanywa na mwenzako, hiyo imethibitishwa na Staa wa filamu nchini Ghana, Kwaku Misa baada ya kumtaja mkali wa komedi,  DKB kama muigizaji mkali wa vichekesho zaidi nchini humo.
Kauli hiyo ya Kwaku imekuja siku chache baada ya kuwepo na taarifa kuwa Mke wa Rais wa Nchi hiyo, Nana Konadu kusikika akiponda staili ya uchekeshaji ya DKB kuwa ni mbaya na haifurahishi.
“ Kwangu mimi DKB ndio mkali wa komedi hapa Nollywood, nimekuwa katika tasnia hii kwa muda mrefu na pia nafanya vipindi vya TV naelewa na kutambua kazi kubwa anayoifanya, ni mbunifu na mjanja wa maneno, ni bora leo hadi kesho,” anasema Kwaku.


0 Comments: