Chicago, Marekani
NYOTA wa kibao cha Like I Would Zayn Malik amefichua siri kuwa alikuwa akiugua ugonjwa wa ajabu wa kushindwa kula katika miezi yake ya mwisho akiwa ndani ya kundi la One Direction.
“Kama nikivuta picha na kujiangalia jinsi nilivyokuwa Novemba 2014, ndiyo nanagundua ni kwa jinsi gani nilivyokuwa naumwa, kitu hiki sikuwahi kukiweka hadharani hapo kabla.Kiukweli baada yakuweka wazi kuwa ninaondoka ndani ya bendi niliumwa mno,”anasema.
Anasema alikuwa akipitia katika kipindi kigumu huku ikimlazimu wakati mwingine kukaa hadi siku mbili au tatu mfululizo bila ya kula kitu chochote.
Malik alihama bendi yake ya mwaka 2015 baada ya kutoshiriki katika shughuli nyingi za kibendi ikisemekana kuwa alikuwa ana ‘stress’.
Hata hivyo, nyota huyo wa Pop alikuja kubainika anafanya kazi zake binafsi huku akitoa albam yake ya kwanza iliyojulikana kwa jina la Mind of Mine mapema mwaka huu.
0 Comments:
Post a Comment