Sunday, March 5, 2017

SIO KILA MSANII ANATAKA KUFIKA MBELE KIMATAIFA-AY

RAPA mwenye mafanikio nchini AY amesema siyo kila msanii amekuwa na malengo ya kutoboa nje ya nchi kwani wengine mipango yao ni kuhakikisha wanateka soko la Bongo pekee.


Akizungumza na DJ Show ya Radio One, AY amesema siyo lazima wasanii wote watoke kimataifa kwani hayo ni maamuzi ya mtu kama anataka kuufikisha muziki wake nje ya mipaka ya Bongo au anataka aendelee kuhit ndani ya mipaka yetu peke.
“ Unajua kila mtu ana mipango yake kwenye muziki wake, kama malengo ya msanii ni kufika levo za kimataifa basi inambidi apambane na kuhakikisha anatoboa kweli, ni kama ilivyo kwenye soka kuna mchezaji anapenda kucheza ligi za ndani mwingine kucheza soka la kimataifa, hivyo hivyo kwenye muziki pia,” Anasema AY.

0 Comments: