MWIGIZAJI wa filamu nchini Kajala Masanja 'amewabwatukia' wale wote wanaosema eti ameshindwa kumlea binti yake ' Paula' na kudai anatamani awaoneshe watu hao malezi anayompatia binti yake huyo.
Kajala aliyasema hayo wiki hii wakati akipiga stori na eNewz, ambapo ameweka wazi hawezi kushindwa kumlea mtoto wake na malezi anayompatia binti yake ni tofauti na yale watu wanayoyazungumzia katika mitandao ya kijamii.
Anasema hajashindwa kumlea mtoto wake na anatamani wangekuwa wanaona malezi ambayo amekuwa akimpatia Paula kwani kila wanachokiona na kukisikia kwenye mitandao ni tofauti sana na ninavyomlea.
Pia staa huyo ameongeza serikali inapaswa kushughulikia matatizo yanayotolewa na watumiaji wa mitandao kwa umakini wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kuweka nguvu ya kutosha.
0 Comments:
Post a Comment