Thursday, March 2, 2017

Aunty Ezekiel na Hamorapa wazidi kutupiana madongo


KIMENUKA! Diva kutoka familia ya Wasafi, Aunty Ezekiel amekinukisha tena baada ya kuibuka na kumshambulia msanii anaetawala vichwa vya habari hivi sasa, Hamorapa kuwa hana kipaji cha muziki na wala hafai kuimba.

Aunty amebainisha kuwa haoni kipaji chochote cha muziki alichonacho Hamorapa na katu hawezi kupoteza muda wake kumsikiliza au kuangalia video za rapa huyo.
“ Hana kipaji chochote sana sana naona anatumia nguvu nyingi kuimba tu, huo muda wa kumsikiliza ni bora nikafanya shughuli nyingine,” Anasema Aunty.
Kuonesha kwamba sasa kunafuka moto baina ya Hamorapa na Aunty, Rapa huyo ameachia wimbo wake mpya unaoitwa Kiboko ya Mabishoo ambao amemshirikisha Juma Nature, ambapo ameutumia kumchana dansa wa Wasafi ambaye ni mume wa Aunty, Mose Iyobo.

0 Comments: