Wednesday, March 1, 2017

Adele kufunga ndoa ndani ya mwaka huu

London, Uingereza
MWAKA 2017 unaweza ukawa ni neema kwa mwanamuziki nyota na mwenye uzuri wake nchini Adele.

Mwimbaji huyo anatarajia kufunga ndoa ndani ya mwaka huu na mpenzi wake wa muda mrefu, Simon Konecki aliyedumu naye kwa miaka mitano kwenye mahusiano.
Imedaiwa kuwa Simon (42) alimvalisha kwa siri pete ya uchumba ya dhahabu Adele (28) mwezi Oktoba mwaka jana.
“Kwa sasa baada ya pete hiyo kifuatacho ni ndoa ambayo inategemewa kufanyika siku yoyote,”kilisema chanzo cha karibu na familia hiyo.
Inasadikika kuwa wawili hao watatarajiwa kuishi East Sussex, Uingereza baada ya ndoa yao kwa kuwa ni sehemu ambayo Simon amekuwa akiipenda zaidi.



0 Comments: