Monday, February 27, 2017

Maprodyuza watano waliohama studio Bongo

LEO nakuletea orodha ya watayarishaji watano wa muziki wa Bongo Fleva ambao walihama studio walizokuwa wakizifanyia kazi na kwenda kufungua zao au kuajiriwa kwingine.


Lamar

Mwanzoni alikuwa akifanya kazi zake 41 Recods, studio inayomilikiwa na Dunga, lakini baadae alihama na kwenda kufungua studio yake 'Fish Crab' ambayo hadi sasa ndipo kazi zake zinatokea.
Pancho

Alitambulika kwenye 'game' akiwa anafanya zake pale Dhahabu Records, kwa sasa inajulikana kama 'Studio 4.12' ambayo inamilikiwa na msanii Dully Sykes. Baadae alihama na kwenda B'Hits na kuungana na prodyuza Hermy B ambaye ndiye mmiliki.

Nahreel

Alishafanya kazi kwenye studio nyingi ikiwemo Kama Kawa Recods, na mwishoni Switch Records inayomilikiwa na Quick Rocka.Baadae aliamua kwenda kufungua studio yake inajulikana kama 'The Industry' ambayo yupo hadi sasa.

Mr T Touch

Awali alikuwa akiporomosha midundo studio ya Free Nation inayomilikiwa na msanii Ney Wamitego. Mwishoni mwa mwaka jana alitimuka na kwenda kufungua studio yake ijulikanayo kama Touchez Sound.

Luffa

Bado ni prodyuza mchanga kwenye 'game' mwanzoni alikuwa anafanya kazi zake pale Switch Records inayomilikiwa na Quick Rocka. Mapema mwezi huu alihamishia makazi yake Wanene Entertainment.

0 Comments: