STAA wa filam nchini, Uwoya anasema siku za karibuni anasema yeye anayo hofu ya Mungu na anapenda kusali lakini linapokuja suala la kazi yake anaona inamsumbua kwenye imani yake.
"Kila siku asubuhi nikiamka huwa inabidi kumuomba msamaha Mungu wangu ndiyo niendelee na kazi," anasema Uwoya na kuongeza anatamani siku moja awe na kanisa lake.
Kuhusu dawa za kulevya, anasema hajawahi kutumia na wala hatumii na kueleza hata dini yake hairuhusu kutumia dawa hizo lakini pombe anakunywa.
"Situmii dawa za kulevya lakini nakunywa bia, dini yangu haizuii kunywa, nina uwezo wa kumaliza hata kreti nzima, hata mapadre kwenye dini yetu wanakunywa, lakini hairuhusiwi kulewa,"anasema.
0 Comments:
Post a Comment