Tuesday, January 3, 2017

Amanda afurahia msimu wa Sikukuu

KIMWANA mwenye vyeo kibao katika ardhi ya Madiba, Amanda du-Pont amesema hakuna nyakati nzuri kwake kama kipindi cha Krismasi na mwaka mpya kwani hutumia kujumuika na ndugu na familia yake.

Amanda ambaye licha ya kuwa muigizaji pia ni mtangazaji wa Tv, anasema kwa muda wa mwaka mzima huwa yupo bize sana lakini kila ifikapo mwisho wa mwaka huhakikisha anaacha kila kitu ili kujumuika na familia yake.
“Ni Krismasi pekee ndio napata nafasi ya kukaa meza moja na familia yangu tukapata chakula kwa pamoja, ni kipindi ambacho hutokea mara moja kwa mwaka kwa sababu kila mmoja yupo bize lakini sikukuu hizi huwa zinatuleta pamoja,”anasema kimwana huyo.
Kuhusu zawadi gani angetamani kupewa katika msimu huu wa sikukuu, “Ooh jibu ni rahisi tu sitaki mti wa Krisimasi wala maua nachohitaji ni simu ya Iphone 7 Plus tu hahahah,” anadokeza.


0 Comments: