Baada ya kuachia video/wimbo wake wa kwanza ‘NOMA’ miezi michache iliyopita, msanii Coyo ambaye ni mwenyeji wa jiji la
miamba, Mwanza anatambulisha kazi yake mpya NJOO BAADAE, ikiwa
ni ya pili kuachiwa akiwa chini ya usimamizi wa Tetemesha Entertainment.
Akizungumzia wimbo
wake mpya, Coyo anasema, “NJOO BAADAE ni wimbo unaozungumzia maisha ya kila
siku ya vijana”.
“Ninamzungumzia mtu anayekuchanganyia mafaili kwa stori (umbea) muda ambao unamishe
zako ambazo haziendani na stori zake, hivyo
unaamua kumchana habari hizo apeleke kwa zinaowahusu au aje baadae.” Ameongeza.
NJOO BAADAE imeandikwa na Coyo ambaye pia amefanya viitikio vya kuimba, na muziki wake umeandaliwa na watayarishaji watatu, Mr T
Touch, mtayarishaji mpya aitwaye Daydream pamoja na KidBway chini ya usimamizi
wa Tetemesha Ent.
Wimbo wa NJOO BAADAE pamoja na Instrumental vimeambatanishwa
hapa, share na wengine kadri uwezavyo.
Tazama mashahiri ya NJOO
BADAAE hapa: https://youtu.be/llLrVJvPeok
Tazama video yake
iliyopita ‘NOMA’ hapa: https://youtu.be/VEPUTJL_Tj8
Editor’s Notes:
·
Kwa sasa Coyo
amehamishia makazi yake jijini Dar es salaam ili kurahisisha shughuli zake za
kimuziki
Tafsiri ya mistari ya kisukuma kwenye verse ya kwanza na ya
pili.
·
Wabeja
(Asante)
·
Lekaga tuja( acha dharau)
·
Nale na shida shane (nipo na shida zangu)
·
We nitakupeja
(we nitakukimbiza/kufukuza)
KWA MAHOJIANO:
COYO: +255712228242
MITANDAO YA KIJAMII:
www.instagram/ coyotz1
MANAGEMENT CONTACT:
Email: sandumpanda@gmail.com
Call: +255784131073
0 Comments:
Post a Comment